NJIAPANDA; NIFANYE NINI WIVU WA MWANANGU UMENIFANYA KUPEWA TALAKA?
Mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka miwili sasa. Mimi na mume wangu tuko vizuri,a naanihudumia na hakuna shida yoyote, mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulishindwana na kuachana, yeye akaenda kua mwanamke mwingine na mimi nikaolewa, Baba wa mtoto anahudumia vizuri mtoto wake na kila likizo anaenda kukaa kwake. Sababu ya kuja kwako ni hivi, mwanangu nahisi kumpoteza, mke wake ni mtu mzuri sana kwa mwanangu. Mwanangu ana miaka mitano, lakini kila akirudi kutoka likizo kwa Baba yake anakua na furaha na anatamani kubaki huko huko. Najaribu kumchunguza kama Mama yake wa kambo anamtesa lakini wapi, anaonekana anampenda. Naumia sana, mwanzo nilikua naumia na picha ambazo alikua anapest Baba yake. Labda mwanangu ameenda wametoka wote na mkewe, wanacheza, mtoto wangu anaonekana kuwa na furaha akiwa na yule Mama kuliko hata mimi. Hali hiyo ilikua inaniumiza sana kwani naona kama wana raha kuliko mimi. Baaada ya kuumia sana nikaona ili wasiwe ...